Dira na Dhamira
Dira na Dhamira
Dira/Maono
Kuwa mdhibiti kinara wa taaluma za Ubunifu majengo, ukadiriaji majenzi na taaluma zinazohusiana katika kanda.
Dhamira
Kudhibiti taaluma za Ubunifu majengo, ukadiriaji majenzi na taaluma zinazohusiana kwa njia ya:
- kusajili wataalamu,
- kutoa mafunzo,
- kukuza taaluma,
- kufuatilia na kusimamia viwango vya kitaaluma,
- na kuhakikisha kulindwa kwa taaluma kwa ajili ya mazingira endelevu ya ujenzi na ulinzi wa umma.
Maadili Muhimu
- Uadilifu (Integrity): Tunatoa huduma zetu kwa kiwango cha juu cha maadili, siri, uaminifu na uwazi.
- Utaalamu (Professionalism): Tunatekeleza majukumu yetu kwa viwango vya juu vya kitaaluma, maadili na ujuzi.
- Uwazi na Uwajibikaji (Transparency and Accountability): Tunatekeleza majukumu yetu kwa uwazi na uwajibikaji kikamilifu kwa matendo yetu.
- Haki na Usawa (Impartiality): Tumejizatiti kuwa wa haki, sawa, bila upendeleo, na wa kimsingi katika utoaji wa huduma.
- Ushirikiano na Kazi ya Pamoja (Teamwork and Collaboration): Tunaahidi kushirikiana kwa mtandao na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yetu.
- Kujali Mteja (Customer Focused): Tumejizatiti kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wateja