Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

Bodi ya Wakurugenzi

Bodi ya Wakurugenzi ya AQRB ni chombo cha juu cha uongozi wa Bodi kinachoongoza, kusimamia na kutoa maamuzi ya kimkakati kwa mujibu wa Cap 269, Revised Edition 2023.
Bodi inahakikisha kuwa AQRB inatekeleza majukumu yake ya kisheria kwa ufanisi, uwazi na kwa maslahi ya umma.
Majukumu ya Bodi ya Wakurugenzi ya AQRB
1. Kuweka Sera na Mwelekeo wa Kimkakati - Kuandaa na kuidhinisha sera, mikakati, na mipango ya muda mfupi na mrefu ya Bodi.
2. Kusimamia Utekelezaji wa Majukumu ya Kisheria -Kuhakikisha usajili, udhibiti na usimamizi wa taaluma za usanifu majengo, ukadiriaji majenzi na taaluma shirikishi unafanyika kwa mujibu wa sheria.
3. Kuamua Maombi ya Usajili - Kupitia na kuidhinisha au kukataa maombi ya usajili wa wataalamu na kampuni kwa mujibu wa sheria na kanuni.
4. Kusimamia Nidhamu na Maadili ya Kitaaluma -Kushughulikia masuala ya kinidhamu, malalamiko, na ukiukwaji wa maadili ya kitaaluma.
5. Kuidhinisha Bajeti na Kusimamia Fedha -Kupitia na kuidhinisha bajeti ya mwaka, ada za usajili, na kuhakikisha matumizi ya rasilimali yanafanyika kwa uwajibikaji.
6. Kusimamia Menejimenti ya Bodi -Kusimamia utendaji wa Msajili na Menejimenti ili kuhakikisha malengo ya Bodi yanafikiwa.
7. Kulinda Maslahi ya Umma -Kuhakikisha huduma za wataalamu zinatekelezwa kwa viwango vya kitaaluma vinavyolinda usalama, ubora, na maslahi ya wananchi.
Hakuna Taarifa kwa sasa